• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Pakistan zitasimama na kusonga mbele pamoja

    (GMT+08:00) 2015-04-21 16:33:03

    Rais Xi Jinping wa China amesema, China na Pakistan daima zitasonga mbele pamoja, na watu wa China daima watasimama pamoja na wa Pakistan. Rais Xi amesema hayo alipohutubia kikao cha pamoja cha bunge la Pakistan. Amesisitiza kuwa uhusiano wa China na Pakistan umejengwa kwenye msingi wa kuaminiana na kuungana mkono, na nchi hizo mbili zinapaswa kuunga mkono matakwa ya kimsingi ya nchi nyingine, na kusema China inaunga mkono kidhabiti mamlaka ya ardhi ya Pakistan.

    Rais Xi pia amepongeza juhudi za Pakistan katika kupambana na ugaidi, akisema nchi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugaidi na imejitolea kwa kiasi kikubwa katika kutimiza hilo.

    Akizungumzia uhusiano kati ya China na Asia Kusini, rais Xi amesema China ni jirani mkubwa wa nchi za Asia Kusini, na amani na utulivu wa eneo hilo unaendana na matakwa ya China.

    Rais Xi anatarajiwa kuondoka Pakistan baadaye leo na kuelekea nchini Indonesia ambapo atahudhuria mkutano wa Asia na Afrika na shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya mkutano wa Bandung.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako