• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa kwanza wa Mfuko wa Njia ya Hariri wafanya maneno ya China kuwa vitendo

    (GMT+08:00) 2015-04-21 18:03:30

    Mradi wa kwanza wa uwekezaji uliofadhiliwa na Mfuko wa Njia ya Hariri wa China umezinduliwa, ikiwa ni utekelezaji wa Ukanda Mmoja Njia Moja.

    Mradi huo uliozinduliwa jana wakati wa ziara ya rais Xi Jinping wa China nchini Pakistan ni hatua kubwa kwa ushirikiano wa wenzi wa kimkakati wa siku zote kati ya China na Pakistan. Mradi huo unamaanisha kuwa, Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri Baharini ya Karne ya 21 umepiga hatua moja mbele.

    Uwekezaji huu wa dola za kimarekani billioni 1.65 kwenye mradi wa uzalishaji wa umeme wa Karot nchini Pakistan pamoja na miradi mingine ya umeme kwenye kanda hiyo, utaisaidia nchi hiyo kuongeza upatikanaji wa umeme na kuinua uwezo wake kiuchumi.

    Mradi huo pia ni kipaumbele cha ushoroba wa kiuchumi wa China na Pakistan, ambao ni sehemu ya Ukanda Mmoja Njia Moja, mpango uliopendekezwa na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako