• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China awasili Jakarta kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Asia na Afrika na maadhimisho ya miaka 60 ya mkutano wa Bandung

    (GMT+08:00) 2015-04-22 09:54:59

    Rais Xi Jinping wa China leo amewasili Jakarta Indonesia, kutokana na mwaliko wa rais Joko Widodo wa Indonesia. Akiwa huko atahudhuria mkutano wa viongozi wa Asia na Afrika na shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya mkutano wa Bandung,

    Rais Xi ameanza ziara nchini Indonesia baada ya kukamilisha ziara yake nchini Pakistan. Rais Xi amemshuruku waziri mkuu wa Pakistan Bw. Mian Muhammad Nawaz Sharif, serikali ya nchi hiyo na wananchi wake kwa mapokezi mazuri, na kusema ziara hiyo imemfanya ajionee kikamilifu urafiki wa wananchi wa Pakistan kwa China.

    Habari nyingine zinasema, waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Bw. Aminu Bashir Wali ambaye yuko nchini Indonesia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Asia na Afrika, jana alisema nchi za Asia na Afrika zinakabiliwa na changamoto nyingi, na China imefanya kazi muhimu katika kulinda maslahi ya nchi zinazoendelea na makundi yanayoibuka kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako