Jose Mourinho awataka wachezaji wake wasishangilie hadi wakishinda mechi mbili zilizosalia
(GMT+08:00) 2015-04-22 14:28:43
Baada ya Chelsea juzi usiku kuichapa Manchester United 1-0 katika dimba la Stamford Bridge kocha wa Jose Mourinho aliwataka wachezaji wake wanyamaze na wasishangilie kabisa mpaka wakishinda mechi mbili zijazo. Chelsea itakuwa katika Jiji la London wikiendi ijayo kucheza dhidi ya Arsenal ugenini kabla ya kucheza na Leicester City ambayo inapigania isishuke daraja. Mourinho amewataka wachezaji wake waache kushangilia kwa sasa. Kocha huyo alikipongeza kikosi chake kilichocheza juzi dhidi ya Manchester United ambacho kilipata ushindi wake kupitia staa wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard aliyefunga bao murua la tobo akikokota mpira alioupokea kutoka kwa Oscar. Kwa sasa Chelsea inaongoza kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya Arsenal ikiwa na pointi 76 huku Arsenal ikiwa na pointi 66. Matokeo hayo yameiacha Manchester United ikibakiwa na pointi 65 mkononi.