• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bob Arum avunja mkutano wa Manny Pacquiao baada ya kuulizwa swali moja tu

    (GMT+08:00) 2015-04-22 14:29:26
    Meneja wa bondia Manny Pacquiao, Bob Arum ameamua kuvunja mkutano uliokuwa wa mwisho kufanyika kwa Pacquiao kabla ya mdundano wa Mei 2 kati yake na Floyd Mayweather kwasababu hakutaka waandishi wa blog kuhudhuria kwenye mkutano huo. Pacquiao alipaswa kufanya mkutano huo ambao angezungumza na vyombo vya habari kwa mara ya mwisho kabla ya pambano lake litakalofanyika huko Las Vegas lakini Arum alisema huo ni upumbavu na hatimaye kutofanyika. Yalianzia kwa matatizo ya kiufundi, ambapo mkufunzi Freddie Roach hakuwa na sauti na kutosikika vizuri kwa zogo na kuishia kwa Arum kuwakoromea wafanya zogo na hatimaye kuvunja mkutano baada ya kumuona ripota wa Examiner.com, Michael Marley, akiwa wa kwanza kuchaguliwa kuuliza swali na muongozaji. Baadaye Arum alisema ni waandishi maalumu ndio waliopaswa kuhudhuria mkutano huo na kwamba hakutegemea kuona waandishi wa blog wakiwepo mkutanoni.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako