Rwanda imeteuliwa kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Cecafa Challenge Cup, Novemba mwaka huu. Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye amethibitisha uamuzi huo. Rwanda itatumia fainali hizo kujiandaa kwa michuano ya fainali za kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi ya nyumbani, maarufu kama CHAN. Fainali hizo za CHAN, ni za pili kwa ukumbwa kwa wachezaji wanaocheza ligi mbali mbali za nchini mwao barani Afrika.