• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IAAF yasema Russia haitapigwa marufuku kushiriki mashindano ya riadha ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2015-04-22 15:31:46
    Russia haitapigwa marufuku kushiriki kwenye mashindano makubwa kwasababu ya madai ya kutumia dawa za kuongeza nguvu. Kauli hiyo imetolewa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa. Televisheni ya Ujerumani mwaka jana ilionesha makala inayodai kwamba asilimia 99 ya wanariadha wa Russia wanatumia dawa za kuongeza nguvu. Shirikisho hilo pamoja na Shirikia la Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu yanaendelea na uchunguzi. Hata hivyo rais wa Shirikisho la Riadha la Kimataifa Lamine Diack ambaye ataachia ngazi mwezi Agosti baada ya kuwepo madarakani kwa miaka 16 amesema utakuwa upuuzi kama wakipigwa mafuruku kushiriki mashindano. Mwezi Januari Shirika la Kupambana na Dawa za Kuongeza Nguvu la Russia liliwasimamisha wanariadha watano, wakiwemo mabingwa watatu wa Olimpiki. Mwezi huohuo Tetyana Chernova naye alipigwa marufuku ya miaka miwili na shirika hilo la Russia kwa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako