Pambano la Mayweather na Manny Pacquiao tiketi bado hazijaanza kuuzwa
(GMT+08:00) 2015-04-22 15:32:21
Promota Bob Arum bado hajaweza kuelezea kwanini hakuna tiketi zilizoanza kuuzwa katika mauzo ya jumla kwa ajili ya pigano la shoka kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao litakalofanyika Mei 2 huko Las Vegas. MGM Grand ina tiketi 16,500 lakini ni 1,000 tu zinazotarajiwa kuuzwa kwa watu. Mkataba na MGM Grand bado haujasainiwa, huku tiketi pia zikiwa hazijaanza kuuzwa katika kumbi za Las Vegas. Juzi Arum alivunja mkutano na waandishi wa habari kabla hata hajaulizwa maswali. Wakati huohuo jana ilitangazwa kuwa Kenny Bayless, ambaye amechezesha mbalimbali yaliyomshirikisha Mayweather na Pacquiao, atakuwa mtu wa tatu kupanda ulingoni usiku wa pambano. Bayless ameanza kuchezesha pambano lake kwanza mwaka 1997 na anachukuliwa ni refa bora katika ngumi. Katika pambano hilo majaji watakuwa Burt Clements, Dave Moretti na Glenn Feldman.