IAAF yataka marufuku ya Rita Jeptoo iongezwe mara mbili
(GMT+08:00) 2015-04-22 15:33:07
Shirikisho la Riadha la Kimataifa IAAF limeitaka mahakama ya juu ya michezo kuongeza mara mbili adhabu ya marufuku ya Rita Jeptoo baada ya kutumia dawa za kuongeza nguvu, ambayo awali ilikuwa miaka miwili. Lakini Chama cha Riadha cha Kenya kimekata rufaa katika Mahakama ya usuluhishi ya michezo na kutaka abadilishiwe adhabu yake baada ya kupatikana anatumia dawa za kuongeza nguvu. Jeptoo mwenye miaka 34 amekuwa mwanariadha wa kwanza mwenye sifa kubwa kupatikana akitumia dawa hizo, baada ya kupimwa mwezi Septemba. Chama cha Riadha cha Kenya kilimsimamisha kushiriki michezo yote hadi Oktoba mwaka 2016. Mahakama ya usuluhishi imesema IAAF inataka iwe marufuku ya miaka minne kwasababu ya "mazingira ya kukasirisha zaidi". Lakini Jeptoo ambaye anasema labda aliandikiwa dawa hizo hospitali baada ya kupata ajali ya barabarani, anataka kucheleweshwa kwa utekelezaji wa marufuku hiyo na kutarajia kushindana katika mashindano ya mabingwa wa dunia mwezi Agosti.