• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa viongozi wa Asia na Afrika wafunguliwa na rais Xi Jinping wa China ahutubia mkutano huo

    (GMT+08:00) 2015-04-22 17:06:56

    Mkutano wa viongozi wa Asia na Afrika umefunguliwa leo asubuhi huko Jakarta, Indonesia. Viongozi wanaohudhuria mkutano huo wanajadiliana namna ya kurithisha na kutekeleza Moyo wa Bandung, kuhimiza ushirikiano kati ya Asia na Afrika na maendeleo ya pamoja ya nchi za Asia na Afrika. Kauli mbiu ya mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kuhimiza amani na ustawi wa dunia. Rais Xi Jinping wa China alipohutubia mkutano huo, alitoa mapendekezo matatu, na kusisitiza kwamba China itahimiza kithabiti ushirikiano kati ya Asia na Afrika. Fadhili Mpunji ana maelezo zaidi

    Akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa Asia na Afrika uliofanyika mjini Jakarta, Indonesia, rais Xi amesema ushirikiano wa Kusini na Kusini unatakiwa kuwa chini ya msingi wa kuheshimiana na usawa, na amesisitiza kuwa katika hali mpya ya hivi sasa, Moyo wa Bandung bado una nguvu kubwa ya uhai.

    "Tunatakiwa kueneza Moyo wa Bandung, kuingiza mambo mapya kwa moyo huo katika ama hii mpya, kusukuma mbele uhusiano wa kimataifa wa aina mpya juu ya msingi wa kushirikiana na kunufaishana, kuhimiza maendeleo ya utaratibu na mfumo wa kimataifa yawe na mwelekeo wa haki, kuhimiza kujenga jumuiya ya hatma ya pamoja ya binadamu, na kunufaisha watu wa Asia, Afrika pamoja na wa sehemu nyingine duniani."

    Rais Xi amesema, China itaendeleza bila kusita ushirikiano wa Asia na Afrika chini ya mazingira mapya, na kushauri nchi za Asia na Afrika kuimarisha ushirikiano kati yao, kupanua ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuhimiza ushirikiano wa Kusini-Kaskazini.

    "Pande mbalimbali zinatakiwa kushikilia kanuni za kunufaishana, kujiendeleza kwa pamoja, na kuunganisha mikakati ya maendeleo, na kufanya hali ya kusaidiana kiuchumi ya Asia na Afrika kuwa nguvu ya kupata maendeleo yao. Nchi za Asia na Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano kati yao, na vilevile kuzidisha ushirikiano na nchi zinazoendelea za Latin Amerika, Kusini mwa Pacific na sehemu nyingine duniani, kupanua mazungumzo na mawasiliano katika usimamizi wa mambo ya nchi, kuhimiza nchi zilizoendelea kutimiza ahadi ya kutoa misaada na kuzisaidia zaidi nchi zinazoendelea bila ya kuweka masharti ya kisiasa, na kuanzisha uhusiano wa wenzi wa maendeleo duniani wa aina mpya wenye usawa zaidi."

    Rais Xi pia ametangaza kuwa, China itazipatia nchi zilizo nyuma kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kibalozi na China fursa ya kuondolewa kodi kwa asilimia 97 ya bidhaa zinazoagizwa ndani ya mwaka mmoja, na itaendelea kutoa msaada kwa nchi zinazoendelea bila masharti ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako