• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Japan

    (GMT+08:00) 2015-04-22 20:20:07
    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na waziri mkuu wa Japan Bw. Shinzo Abe huko Jakarta, Indonesia, ambapo viongozi hao wawili wamebadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya China na Japan.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi Jinping amesema, suala la kihistoria ni suala kuu linalohusiana na msingi wa kisiasa wa uhusiano wa China na Japan, na China inaitaka Japan izingatie ufuatiliaji wa nchi jirani, na kuangalia kwa ufasaha historia.

    Amesisitiza kuwa, China inatumai Japan itajiendeleza kwa njia ya amani pamoja na China, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa kikanda na dunia nzima.

    Naye Bw. Abe amesema, anakubali kuwa maendeleo ya Japan na ya China hayatishiani, na Japan inapenda kuhimiza mawasiliano na mazungumzo kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali, na kuongeza maelewano kati ya watu wao. Pia amesema Japan inapenda kujadiliana na China kuhusu suala la Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia AIIB.

    Rais Xi leo pia amekutana na rais U hain Sein wa Myanmar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako