• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya mkutano wa baraza la Asia na Afrika

    (GMT+08:00) 2015-04-23 10:40:50

    Viongozi wa nchi za Asia na Afrika jana walikusanyika Jakarta Indonesia kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 60 tangu kufunguliwa kwa mkutano wa baraza la Asia na Afrika, yaani mkutano wa Bandung. Rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kwenye mkutano huo, na kueleza sura mpya kuhusu jinsi nchi zinazoendelea zinavyoweza kushikamana na kushirikiana ili kufanya kazi kubwa zaidi na kuhimiza maendeleo yenye uwiano duniani katika zama mpya. Pia ameahidi kuwa China daima itakuwa rafiki na mwenzi wa dhati wa nchi zinazoendelea.

    Katika miaka 60 iliyopita, mabara ya Asia na Afrika yamepata maendeleo makubwa sana, na hadhi zao zinainuka siku hadi siku. Idadi ya watu katika mabara hayo mawili inachukua robo tatu ya watu wote duniani, na idadi ya nchi imezidi nusu katika nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, hivyo ushirikiano kati ya Asia na Afrika umekuwa na umuhimu mkubwa zaidi siku hadi siku.

    Wanataaluma mbalimbali duniani wamekuwa wakitoa maoni yao kuhusiana na umuhimu wa mkutano huo na maadhimisho hayo. Naibu mkuu wa taasisi ya utafiti wa suala la kimataifa ya China Ruan Zongze amesema, zamani nguvu za nchi za Asia na Afrika ilikuwa dhaifu, lakini kadiri nchi zinazoendelea zinavyoendelea, ufuatiliaji wa uchumi wa dunia umehamishwa, na nguvu za nchi za Asia na Afrika imeimarishwa katika uhusiano wa kimataifa. Rais Xi amependekeza kuenzi moyo wa mkutano wa Bandung, ili kuhimiza utaratibu na mfumo wa kimataifa uendelezwe kwa haki zaidi. Hii inamaanisha kuwa katika siku za baadaye nchi za Asia na Afrika zitafanya kazi kubwa zaidi na kuwa na sauti kubwa zaidi katika jukwaa la kimataifa.

    Rais Xi pia amesema moyo wa Bandung si kama tu unafaa kwa ushirikiano kati ya Asia na Afrika na ushirikiano kati ya kusini na kusini, bali pia una umuhimu mkubwa katika kuhimiza ushirikiano kati ya kusini na kaskazini.

    Bw. Ruan Zongze pia anaona kuwa, mapendekezo ya ushirikiano kati ya kusini na kaskazini yameonesha upeo mkubwa na wazo shirikishi la China. Amesema ushirikiano kati ya kusini na kusini kwa sasa hautoshi. Nchi zinazoendelea zinapaswa kushirikiana na nchi za kaskazini na nchi zilizoendelea, katika ushirikiano ambao sio tu unaweza kukabiliana vizuri zaidi na mgogoro, vilevile unaweza kuleta fursa ya maendeleo. Katika kukabiliana na masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, ukosefu wa maliasili, ugaidi na afya ya umma, haviwezi kutegemea nchi za kusini peke yake.

    Rais Xi pia ametoa hatua halisi ya kuhimiza ushirikiano kati ya Asia na Afrika, akisema China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali ili kusukuma mbele ujenzi wa "ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na njia ya hariri ya baharini ya karne 21", na kujenga vizuri kwa pamoja benki ya uwekezaji wa miundo mbinu ya Asia, ili mfuko wa njia ya Hariri ufanye kazi vizuri.

    Dk. Li Renliang wa chuo cha mambo ya utawala cha Thailand amesema hotuba ya rais Xi Jinping inasisitiza kuinua kiwango cha ushirikiano kati ya nchi za Asia na Afrika, na kueleza njia ya ushirikiano na hatua za utekelezaji, na hatua hizo zinaendana na moyo wa Bandung.

    Professa Subah Sheikh wa chuo kikuu cha Baghdad cha Iraq anaona kuwa, hivi sasa dunia inakabiliana na masuala mengi ya kimataifa, utatuzi wa masuala hayo unahitaji kujenga mtandao wa ushirikiano wa kimataifa. Ni kwa kutekeleza kanuni tano ya kuishi pamoja kwa amani, ushirikiano huo unaweza kutatimizwa.

    Mtaalamu wa mambo ya diplomasia wa chuo kikuu cha Nairobi Bw Patrick Maluki amesema moyo wa Bandung unaotiwa mambo mpya, utaongoza Asia na Afrika kutimiza ustawi wa uchumi, kufufua siasa na maendeleo endelevu ya amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako