• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Zimbabwe wakutana

    (GMT+08:00) 2015-04-23 14:52:00

    Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na rais Robert Mugabe wa Zimbabwe huko Jakarta, Indonesia.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi Jinping amesema, mwaka huu ni mwaka wa 35 tangu China na Zimbabwe zianzishe uhusiano wa kibalozi. Amesema China inaunga mkono juhudi za Zimbabwe katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi, pia itaendelea kuziunga mkono kampuni na idara za kifedha za China kujadiliana na Zimbabwe kuhusu njia ya kukusanya mitaji katika msingi wa kunufaishana na kutoa misaada ya mitaji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika sekta zinazohusu maisha ya wananchi, na pia kushiriki kwenye ujenzi wa maeneo maalum ya kiuchumi nchini Zimbabwe, na kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za kilimo, viwanda vya usindikaji na utengenezaji, elimu, afya na nyinginezo.

    Kwa upande wake, rais Mugabe ameishukuru China kwa kuiunga mkono Zimbabwe katika kulinda uhuru wake wa kisiasa na kuhimiza maendeleo ya uchumi. Zimbabwe inatumai kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati yake na China, ili kuchangia maendeleo ya uchumi na jamii nchini humo.

    Rais Xi pia amekutana na rais Hassan Rouhani wa Iran, na waziri mkuu Hun Sen wa Cambodia.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako