Tiketi za pambano la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao zimeuzwa ndani ya dakika chache ambapo tiketi zimeonekana kwenye mitandao mbalimbali zikiuzwa kwa dola 70,790. Ni tiketi 1000 moja zilizokuwepo kwa watu kwa ajili ya pambano hilo litakalofanyika Mei 2 katika ukumbi wa Las Vegas. Viti vilivyosalia 15,500 vitakwenda kwa wapiganaji, wadhamini na mapromota. Tiketi ya bei ya chini ni dola 1,500, na za juu kidogo ni dola 7,500. Pambano kati ya wawili hao lilipangwa tangu Februari lakini mkataba wa tiketi umemalizwa kusainiwa wiki hii. Lakini ndani ya dakika zikaonekana kwenye mitandao kama vile StubHub ambalo ni soko linalomilikiwa na eBay – ikiwa ya bei chini ni dola 5,270.