• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WUSHU Tanzania kujiandaa kuija China

    (GMT+08:00) 2015-04-24 09:45:22
    Chama cha mchezo wa WUSHU Tanzania TWA leo kinafanya mchujo wa kupata wachezaji watakaokuja China kuhudhuria mafunzo ya mchezo huo. Katibu mkuu wa TWA, Gola Kapipi amesema wachezaji watakaohusika kwenye mchujo huo ni mikoa iliyoleta wachezaji ambao ni mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na Tanga. Kapipi amesema jumla ya wachezaji wapo wanane ambapo mchujo huo utafanyika na kubaki watano ambao watakuja hapa China. Kapipi amesema mchujo huo utafanyika kwa lengo la kuepusha lawama kutoka kwa viongozi wa klabu na wachezaji kuhusu uteuzi wa wachezaji hao. Wachezaji watakaofuzu zoezi hilo, wataondoka Tanzania Mei nne kuja China tayari kwa mafunzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako