• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Man United yalimwa,Chelsea yatoka sare

    (GMT+08:00) 2015-04-27 14:32:06
    Manchester United ilikosa fursa ya kupanda juu ya pointi kumi dhidi ya Liverpool baada ya kulazwa mabao matatu bila na kilabu ya Everton. Manchester United wangeongeza mwanya uliopo kati yao na Liverpool katika kinyanganyiro cha kufuzu kombe la vilabu bingwa Ulaya. Lakini mabao ya James Mc Carthy na John Stone yaliiweka Everton kifua mbele kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika. Kelvin Mereiles aligonga msumari wa mwisho katika jeneza la United alipofunga bao la tatu. Wakati huohuo Chelsea imeimarisha harakati zake za kutaka kushinda ligi ya Uingereza baada ya kutoka sare ya bila kwa bila na Arsenal katika uwanja wa Emirate na hivyo basi kuhakikisha kuwa wanasalia na pointi kumi mbele ya uongozi wa ligi hiyo..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako