• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Dongguan wakaribisha nchi inakopitia njia ya hariri ya baharini kufanya biashara

    (GMT+08:00) 2015-04-29 14:35:23

    Mamlaka ya manispaa ya mji wa Dongguan nchini China imekaribisha nchi inakopitia njia ya hariri ya baharini kujinufaisha na nafasi za kibiashara mjiji humo. Mji huu wa Dongguan uko kusini mwa China Katika mkoa wa Guangdong na una wakaazi millioni kumi hivi. Pato lake la jumla ni zaidi ya Dola bilioni 95.

    Lakini cha muhimu kufahamu ni kwamba mji huu ulikuwa na wakaazi million moja tu kabla ya Sera ya ufunguzi mwaka wa 1978 wengi wao wakiishi kwa kutegemea kilimo.

    Kwa kipindi cha miaka 30 hivi mji huu umeshuudia ukuaji mkubwa wa sekta yak e ya viwanda kama vya, nguo, magari, electroniki na viatu.

    Bidhaa nyingi kwenye soko la kimataifa hutengenezwa hapa kama anavyoeleza Bwana Yuan Baocheng naibu Katibu wa chama cha kikomunisti kwenye mji huu.

    "Mji huu kwa sasa una sekta za kibiashara zipatazo 640,000 na kati ya hizo 150,000 ni za utengenezaji bidhaa. Mji wa Dongguan ni maarufu kote duaniani kutokana na viwanda vyake. Labda kila mmoja wenu ana simu ya kisasa, na nataka kuwaambia pia asilimia 17 ya simu za kisasa zote hutoka hapa mjini Dongguang na hiyo ina maana kwamba simu milioni 230 ziliuzwa kutoka hapa mwaka jana. Pia kila jozi moja la viatu vya michezo duniani hutengenezewa hapa Dongguan. Hapa pia kuna viwanda vinanyitengeza bidhaa za ubora wa Kimataifa kama vile fenicha, vifaa vya kucheza vya watoto na vya teknolojia ya mawasiliano"

    Mji huu ukiwa ni miongoni mwa ile ilioko kwenye njia ya hariri ya baharini ambayo inaishia afrika mashariki ni muhimu kwa kuendeleza mpango ulioanzishwa na rais Xi Jinping wa China wa Kuwa na njia ya Hariri ya baharini ya karne ya 21.

    Njia ya Hariri ni mkondo wa kusafirisha bidhaa kupitia baharini kati ya Asia, ulaya na Afrika.

    Ili kupigia debe njia hiyo serikaki kuu na za mikoa hapa China zinaandaa warsha na hafla zinazojumuisha nchi kwenye njia ya hariri.

    Mji wa Dongguan utaandaa maonyesho ya pili ya nchi zilizoko kwenye njia hiyo mwezi oktoba.

    Kulingana na naibu Katibu wa chama cha kikomunisti Yuan Baocheng maonyesho hayo yatahimiza sekta ya biashara na pia Kuwezesha kampuni za mji wa Dongguan kukutana na wateja wa nchi za njia ya hariri.

    "Maonyesho ya mwaka jana yalivutia zaidi ya waonyesha bidhaa 1,000 kutoka nchi 42 zilizoko kwenye njia ya Hariri ya baharini. Maonyesho ya mwaka huu yatafanyika mwezi Oktoba na tunatarajia kuweka vibanda zaidi kama elfu mbili hivi na tunatarajia idadi ya waonyesha bidhaa wanunuzi kuongezeka "

    Mojawepo wa kampuni nyingi zilizoko hapa ni ile ya kutengeneza malori ya kubeba mafuta na magari kuzima moto.

    Wana masoko kote duniani lakini sasa wana mipango ya kufanya msisitizo kwenye nchi zilizoko katika njia ya hariri ikiwemo Afrika.

    Yang Lei ni afisa wa mipango na ukuaji wa kampuni hiyo ya Yong Qiang nilimuuliza matarajio yake ya kuwepo na njia ya Hariri ya baharini.

    "Kuna mahitaji makubwa ya bidhaa zetu kwenye nchi zilizoko kwenye eneo lote la njia ya hariri ya baharini. Tayari tumefanikiwa kuanza ushirikiano wa kibiashara na Saudi Arabia na Indonesia. Afrika na kusini mashariki mwa Asia ndio masoko tunayolenga sana na tayari tumeuza zaidi ya magari 2000 barani Afrika na kila mwaka tunatuma maafisa wetu wa biashara kwenda Afrika kujadili ushirikiano "

    Kwa sasa kulingana na bwana Yang Lei wanajadili na serikali ya kenya kuuza magari ya kuzima moto ya yuan milioni 800.

    Bwana Bryan Huang naibu mkurungezi wa kitengo cha kimatafa anaelezea zaidi mustakabali wa soko.

    "Pia tuko na ofisi nchini Nigeria na tuna maajneti katika nchi mbalimbali kwa mfano msubiji na Afrika Kusini ambao wanatusaidia kupanua soko letu. Katika siku za baadaye tunatarajia kwamba mauzo yetu barani Afrika yatafikia asilimia 30. Aidha tumekuwa tukiandaa maonyesho barani Afrika ya kuonyesha wateja wetu jinsi ya kukarabati magari tuyowauzia na nimewahi kwenda Msumbiji na Tanzania kwa maonyesho kama hayo"

    Tayari kampuni ya kutengeneza viatu ya ya Huang Jing ambayo inatoka hapa mjini Dongguang imefungua kiwanda nchini Ethiopia ambacho kinazalisha jozi 2, 000 za viatu kila siku za kuuza kwa soko la nje.

    Na sasa kampuni nyingi za mji huu zinatarajia kuongeza mawasiliano na nchi zilizoko njia ya Hariri ya baharini wakati wa maonyesho ya oktoba kupanua mauzo ama kufungua matawi kwenye nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako