• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la vijana la "Ukanda wa kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini katika karne ya 21" lafanyika Uturuki

    (GMT+08:00) 2015-04-29 10:39:59

    Baraza la vijana la "Ukanda wa kiuchumi wa Njia ya Hariri na Njia ya Hariri baharini katika karne ya 21" linaloandaliwa na ubalozi wa China nchini Uturuki jana lilifanyika Ankara, ambapo watu zaidi ya 50 wakiwemo balozi wa China nchini Uturuki Yu Hongyang, mwenyekiti wa shirikisho la baraza la Ankara Obahan Obaoglu, maofisa wa ikulu ya Uturuki, wabunge wa Chama cha CHP pamoja na watu mashuhuri katika jamii ya Uturuki wamehudhuria baraza hilo.

    Kwenye baraza hilo, balozi Yu Hongyang kwanza amefafanua kwa kina undani wa "ukanda mmoja na njia moja", pamoja na kanuni, lengo, wazo na utaratibu wa ushirikiano kwa ajili ya mpango huo. Balozi Yu amesema, China na Uturuki zina maoni ya pamoja ya kisiasa, na zina msingi imara katika mambo ya uchumi na biashara, mawasiliano, nishati na utalii wa kiutamaduni, hivyo anaamini kuwa nchi hizo mbili zitakuwa na mustakabali mzuri katika kutekeleza mpango huo.

    Bw. Obahan Obaoglu amesema, wazo la kimkakati la "ukanda mmoja na njia moja" lina umuhimu mkubwa katika kuzidisha uhusiano kati ya Uturuki na China. Amesema mpango huo utaipa Uturuki fursa muhimu ya maendeleo, na pia utahimiza mawasiliano na ustawi wa nchi mbalimbali za Asia zilizoko kwenye njia ya Hariri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako