Waandamanaji wanaopinga rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa kipindi cha tatu ambao wameanza kuandamana tangu Jumapili huko Bujumbura wamesema wanawashikilia wanamgambo wa zamani wa Interahamwe wa Rwanda.
Interahamwe ni wanamgambo Wahutu wanaolaumiwa kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda ambapo watu laki 8 waliuawa. Mwandamanaji mmoja alisema mpiganaji wa Interahamwe alikamatwa wakati alipokuwa akiongea na simu kwa Kinyarwanda ambapo waandamanaji waligundua kwamba hakujua jina la mahali alipo ambapo maandamano yalikuwa yakifanyika. Amesema awali waliwakamata wawili, lakini polisi walimchukua mmoja na kumpeleka mahali pasipojulikana.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |