• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahadhari ya mnara wa Canton mjini Guanzhou

    (GMT+08:00) 2015-05-01 10:21:23

    Mnara wa tatu kwa ukubwa duniani unapatikana katika mji wa Guangzhou kusini mwa china na ulijengwa mwaka wa 2010.

    Kama anavyoripoti mwandishi wetu Ronald Mutie, kila siku mnara huo unavutia watu wengi wanaopenda kujionea maadhari ya mji kutoka kilele chake.

    Mnara wa canton ndio mrefu zaidi nchini China na una urefu wa Mita 600. Kazi ya ujezi wake ilichukua miaka 5 na ulifunguliwa mwaka wa 2010. Mnara huua pia ndio wa 3 kwa urefu duniani.

    Mbali na urefu wake pia una umbo la kipekee ambalo ni kama la mwanamke anayesimama wima.

    Kuna namna mbili za kufika ghorofa ya juu ya mnara huu-unaweza kupanda kwa ngazi au kutumia kabarau ya mwendo wa kasi.

    Bi. Colisa Gao ni mtoa maelezo kwenye mnara wa canton

    "Kuna lifti sita za mwendo wa kasi kwenye mnara huu na nne kati ya hizo ni za ghorofa mbili, kwa hivyo kwa kila saa kila lifti inaweza kubeba watu 1,400. Leo ni siku ya jumamosi na hivyo kuna familia nyingi na watalii ambao wamekuja kutembelea mnara. Vilevile, maonyesho ya Canton ambayo yanaendelea pia yanaleta watalii wengi. "

    Lifti ni kubwa na inaweza kubeba watu 20 kwa safari moja na inapanda kwa mwendo wa mita tano kwa sekunde moja tu na inachukua chini ya dakika mbili kufika kilele cha mita 600.

    Ukiwa kwenye kilele cha mnara huu unaweza kuona karibu maeneo yote ya mji wa kibiashara was Guangzhou.

    Na ukiamua kupanda kwakutumia ngazi itakuchukua karibu saa moja kufika kileleni ikitegemea na kasi yako lakini pia kufanya hivyo ni jambo la kihistoria kama anavyosema Bi. Colisa.

    "kwa jumla kuna hatua elfu moja tisini na sita na jina lake maarufu ni Sky walk. Baadhi ya watalii wanaokuja hapa huchagua kupanda kwa ngazi kwa sababu wanaweza kutazama mji wa Guangzhou, bali pia ni njia moja ya kufanya mazoezi . mwongozaji watalii wa mnara huo anashauri kupanda kwa ngazi. Kwa sababu ngazi zipo eneo la kati kati mwa nguzo za chuma na hivyo unapopanda utapata hewa safi na kujihisi vizuri "

    Pia kwenye kilele cha mnara kuna kivutio kingine, vigari vinavyozunguka taratibu kwenye ukingo wa nje. Vigari hivi vimeundwa kwa glasi na ukiwa ndani unaweza kutazama mji ulio chini yako.

    Wapenzi wanapenda sehemu ya vigari na mara nyingi vijana hupendekeza ndoa wakiwa hapa.

    Kila siku mamia ama maelfu ya watu kwenye mnara huu na hilo linaweza kudhihirika kutikana na wingi wa watu kutoka maeneo mbali mbali duniani.

    Usiku mnara wa Canton una mwanga ambao unabadilisha rangi na hivyo kuweza kuonekana maridadi.

    Kwa hivyo siku moja ukifika mjini Guangzhou usisahahu kutembelea mnara wa canton.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako