• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Saudi Arabia lapambana na wapiganaji wa kundi la Houthi

    (GMT+08:00) 2015-05-01 19:25:56

    Wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia imesema, wanajeshi watatu wa jeshi la nchi hiyo wameuawa katika mapigano makali kati ya jeshi hilo na wapiganaji wa kundi la Houthi baada ya wapiganaji hao kushambulia kituo cha polisi kilicho karibu na mpaka wa Yemen na Saudi Arabia.

    Habari nyingine zinasema baraza la ushirikiano la nchi za Ghuba limesisitiza kuwa mazungumzo yanayolenga kumaliza mapigano ya ndani nchini Yemen yafanyike Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, na si sehemu isiyopendelea upande wowote kama ilivyopendekezwa na Iran.

    Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa baraza hilo ikiwemo Saudi Arabia, Kuwait, Falme za Kiarabu, Qatar, Oman na Bahrain walifanya mkutano huko Riyadh kujadili suala la Yemen. Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo inasema, baraza hilo limesisitiza tena kuunga mkono matakwa ya serikali ya Yemen kuhusu kufanya mazungumzo ya amani mjini Riyadh chini ya uratibu wa baraza hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako