• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Azam FC kuchuana na Yanga kwenye ligi ya Vodacom Tanzania

    (GMT+08:00) 2015-05-06 14:23:20
    Wenyeji timu ya Azam FC nchini Tanzania leo watawakaribisha Mabingwa wapya wa ligi hiyo msimu huu, timu ya Young Africans kutoana jasho kwenye ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

    Refa Jacob Adongo kutoka Mara, akisaidiwa na washika vibendera Frednand Chacha (Mwanza), Hellen Mduma (Dar es Salaam), ndio watakaoendesha michezo wa leo.

    Hata hivyo, kwa Yanga, itakuwa ni kama kukamilisha ratiba wakati Azam wanahitaji ushindi katika vita kati yao na Simba ya kugombania nafasi ya pili.

    Bingwa, ambao ni Yanga watawaikilisha nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa afrika wakati mshindi wa pili (kati ya Azam na Simba) wataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako