• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waamuzi wa kandanda ya kike wa Tanzania wateuliwa

    (GMT+08:00) 2015-05-07 14:22:54
    Waamuzi wa Tanzania watakaochezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake U-20 mwaka 2016 kati ya Congo DR dhidi ya Gabon hatimaye wameteuliwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF.

    Jonesia Rukya ameteuliwa kama mwamuzi wa kati, akisaidiwa na washika vibendera, Dalila Jafari na Sophia Mtongoli huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma.

    Mashindano hayo yatafanyika Jumamosi ijayo jijini Kinshasa.

    Wakati huo huo Elizabeth Kalinga ameteuliwa kuwa kamisaa wa mchezo kati ya Kenya dhidi ya Botswana kuwania kufuzu kwa michuano ya Olympiki, mchezo utakaofanyika Mei 31, 2015 nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako