• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juventus watangulia na ushindi kwenye dimba la ubingwa wa ulaya

    (GMT+08:00) 2015-05-07 14:36:21
    Mchezo wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya kati ya Juventus ya Italia dhidi ya Real Madrid ya Hispania umefanyika jana usiku kwa Juve kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

    Juventus wenyeji wa pambano hilo walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa Alvaro Morata.

    Hata hivyo Cristiano Ronaldo alisawazisha katika dakika ya 27. Matokeo yaliyodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

    Juventus walipata goli tena katika dakika ya 57, kutokana na mpira wa adhabu ya penalti, ambapo Carlos Tevez aliifungia timu yake. Hadi kipenga cha mwisho, Juventus 2, Real Madrid mabingwa watetezi 1. Timu hizo zitarudiana tarehe 13 Mei katika uwanja wa Bernabeu, mjini Madrid.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako