• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Azama FC yailaza Yanga FC 2-1

    (GMT+08:00) 2015-05-07 14:36:45
    Timu ya Azam FC hatimaye imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Yanga SC katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Mbrazil Andrey Coutinho alitangulia kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya 14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85.

    Sasa Yanga, wataiwakilisha Tanzania katika Kombe la Afrika mwakani nayo Azam itashiriki kombe la Shirikisho na kuifanya Simba, moja ya klabu kongwe, kuwa nje ya mashindano ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 3 mfululizo

    Mechi ya jana ilikuwa ni ya kukamilisha ratiba tu kwa Yanga, ambao wamekuwa mabingwa wiki moja iliyopita.

    Simba haitaweza tena kuifikia Azam, ambayo kwa ushindi wao dhidi ya Yanga, wamefikisha pointi 48, wakati Simba, hata akishinda mechi yake iliyobaki dhidi ya JKT Ruvu itafikisha pointi 47.

    Ushindi huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako