• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Adebayor alalamikia masaibu kutoka kwa familia yake.

    (GMT+08:00) 2015-05-07 14:37:23
    Mwanasoka Emmanuel Adebayor anayechezea klabu ya Tottenham ameamua kuanika wazi masaibu yanayomkumba ya kifamilia.

    Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook, Adebayor alieleza jinsi jamaa zake wa karibu wamekuwa wakitumia mali yake kwa kuharibu bila ya kuzingatia anavyohangaika kuichuma.

    Alieleza kuwa akiwa na umri wa miaka 17, alipolipwa mshahara wa kwanza, alijenga jumba la kifahari ili kuhakikisha mamake na dunguze wanaishi maisha mazuri ila hakutarajia kuwa dadake angelikuja kuikodisha nyumba hiyo bila ya yeye kujua.

    Adebayor ambaye amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika, ameshangaza ulimwengu kwa kulalama jinsi familia yake imekuwa ikimfyonza na kumfanya kugharamia kila kitu bila kumhurumia hata kidogo.

    Mchezaji huyo amelalamika kuwa licha ya kuwasaidia jamaa zake, hamna lolote ambalo amefaidika nalo licha ya ukarimu wake.

    Adebayor alisema kuwa ameamua kufunguka ili kuwasadia wanadamu wengine popote waliko duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako