• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha Taifa stars chatangazwa kuchuana na Misri, Uganda

    (GMT+08:00) 2015-05-08 14:17:46
    Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 28. Kikosi hicho kitaingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwenye AFCON na CHAN mwezi Juni mwaka huu. katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na kisha kuchagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini. Kikosi hicho kitacheza mechi yake ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri Juni 13 nchini Misri, na kisha kucheza na Uganda jijini Dar es Salaam Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN. Kuelekea katika mchezo wake na Uganda, iliyo nafasi ya 71 katika viwango vya dunia vya FIFA, Nooij amesema kuwa michuano ya Cosafa Cup itakayochezwa Afrika ya Kusini Mei 17 itaisaidia kujiandaa na mechi hiyo pamoja na ile ya mapharao wa Misri. Uganda imealikwa nchini Rwanda katika mashindano maalumu ya kukumbuka wanamichezo waliouawa mwaka 1994 katika mauaji ya kimbali.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako