• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yamweka Mkuu wa al-Jazeera Pakistan kwenye ordha ya wanachama wa al-Qaeda

    (GMT+08:00) 2015-05-09 19:18:12

    Serikali ya Marekani imemtaja mkuu wa kituo cha Al-jazeera nchini Pakistan kama mwanachama wa kundi la al-Qaeda na kumweka kwenye orodha ya watuhumiwa wa ugaidi.

    Ripoti ya Jarida la Intercept la mtandaoni limesema Ahmad Muaffaq Zaidan ambaye ni raia wa Syria, siku zote amefanya kazi akifuatilia habari za Taliban na al-Qaeda na kuwahoji viongozi wakuu wa al-Qaeda akiwemo Osama Bin Laden.

    Mwaka wa 2012 Idara ya usalama wa kitaifa nchini Marekani ilionyesha picha za Zaidan na jina lake likiwa miongoni mwa orodha ya wanaofuatiliwa kwa tuhuma za ugaidi na pia kumtaja kama mwanachama wa Muslim Brotherhood.

    Lakini kwenye mahojiano na jarida la Intercept Zaidan alikana madai ya kuwa mwanachama wa al-Qaeda ama Muslim Brotherhood.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako