• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juhudi za Real Madrid kubeba ushindi zazidi kugonga mwamba

    (GMT+08:00) 2015-05-11 14:05:29
    Kilabu ya Real Madrid iligonga mwamba wa goli mara tatu huku nyota wake Christiano Ronaldo akikosa penalti na hivyo basi kupata sare ya 2-2 na timu ya Valencia hatua iliyodidimiza matumaini yao ya kubeba taji la ligi hiyo. Real ambayo ilikuwa imeshafungwa magoli 2-0 ilikjikurupusha kwa kusawazisha magoli mawili na hatimaye kupata sare hiyo na hivyo kuweka pengo la pointi nne kati yao na viongozi wa sasa Barcelona huku ikiwa imesaliwa na mechi mbili. Paco Alcacer aliipatia uongozi Valencia iliyo nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kabla ya Javi Fuego kufunga la pili. Mkwaju wa penalti uliopigwa na Ronaldo uliokolewa kabla ya Pepe kufunga bao la kwanza na Isco kuongeza bao la kusawazisha. Real Madrid pia ilipata pigo jingine baada ya kumpoteza Tony Kroos baada ya kupata jeraha katikati ya kipindi cha kwanza.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako