• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF yakubali kuwa mwenyeji wa michuano ya Kagame

    (GMT+08:00) 2015-05-11 14:07:19
    Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) limekubali kuwa mwenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya vilabu inayojulikana kama Kagame Cup. Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndio wamiliki wa mashindano haya na hutoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki, watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo baadaye mwezi huu au mapema mwezi ujao. Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema uamuzi wa kukubali kuwa mwenyeji umetolewa na shirikisho hilo mapema Jumapili baada ya kuombwa na Cecafa. Michuano hii inatarajiwa kufanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 Julai mpaka Agosti 2 mwaka 2015. Michuano hiyo inadhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame na hufanyika kila mwaka katika nchi wanachama wa ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati. Rwanda ndio ilikuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka jana inayohusisha vilabu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako