• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Haile Gebrselassie aamua kustaafu mbio za ushindani

    (GMT+08:00) 2015-05-11 14:07:48
    Haile Gebrselassie ametamka bayana kustaafu mbio za ushindani. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka arobaini na miwili mwenye asili ya nchi ya Ethiopia amethibitisha maamuzi yake hayo, na hii ni mara baada ya kuhitimisha mbio za kumi na sita za Great Manchester mapema Jumapili. Maamuzi haya yanahitimisha safari ya miaka ishirini na tano ya kukimbia safari ambayo iliwahi kumpatia medali mbili za dhahabu za michuano ya Olympic, ushindi wa mara nane wa dunia wa riadha na kuweka rekodi duniani ya kufanya vyema mara ishirini na saba katika mbio kubwa duniani. Mwenyewe Haile Gebrselassie anasema kwamba anastaafu mbio za ushindani, sio kustaafu kukimbia. Gebrselassie anabakia kuwa mkimbiaji mwenye rekodi ya kipekee tena mashuhuri katika mbio za mita elfu mbili duniani alizozimaliza kwa muda wa saa moja. Suala la kutaka kustaafu riadha alilisema miaka mitano iliyopita na ni baada ya kupata ajali michezoni lakini akarejea katika mbio miezi kadhaa baadaye.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako