• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Carlo Ancelotti asema ajenti wa Bale ni kidomodomo sana.

    (GMT+08:00) 2015-05-14 16:14:48
    Mkufunzi wa kilabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amemtaka ajenti wa mchezaji Gareth Bale kufunga mdomo wake baada ya kusema kuwa wachezaji wenzake hawampigi pasii vya kutosha. Jonathan Barnet amesema kuwa mshambuliaji huyo wa Wales anataabika kwa kuwa hapati usaidizi kutoka kwa wenzake. Ancelotti alisema huu ni ulimwengu ambao watu wengi huzungumza na mara nyengine huzungumza kupitia kiasi. Amesisitiza kuwa Bale hajawahi kuwa na matatizo na wachezaji wenzake na wenzake pia hawajawahi kuwa na matatizo naye. Bale ndiye mchezaji aliye ghali mno baada ya kusajiliwa kwa kitita cha pauni miloni 85.3 kutoka klabu ya Tottenham katika ligi ya Uingereza mwaka 2013.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako