• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barcelona na Juventus kukutana kwenye fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya

    (GMT+08:00) 2015-05-14 16:16:57
    Miamba ya soka ya Hispania Barcelona, wamefanikiwa kutinga fainali baada ya kuibwaga Bayern Munich kwa jumla ya mabao 5-3 yaliyopatikana katika mikondo yote miwili waliyokutana kwenye hatua ya nusu fainali. Katika mchezo wa usiku wa kuamkia jana ambao ulipigwa ndani ya dimba la Allinza Arena, Bayern walipaswa kushinda magoli manne kwa bila ili kupata tiketi ya kusonga mbele. Lakini mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa the Bavarian walipata 3, huku Barcelona ikipata mabao 2. Aidha katika mchezo uliosakatwa jana usiku kati ya Real Madrid dhidi ya Juventus kwenye dimba la Benabeu, Juventus nao wametoka kifua mbele na kuingia fainali ambapo watakutana na Barcelona katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya. Katika mkondo wa kwanza Real ilifungwa 2 kwa 1na katika mechi ya jana walitoka sare ya 1 kwa 1 na kuifanya Juventus kuwa na jumla ya mabao 3-2. Mechi ya fainali itachezwa Juni 6 huko Berlin.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako