• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pacquiao  alakiwa vizuri Ufilipino licha ya kushindwa na Mayweather

    (GMT+08:00) 2015-05-14 16:17:24
    Bondia Manny Pacquiao amerejea nyumbani kwao Ufilipino baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega huko Marekani ambapo pamoja na kushindwa Floyd Mayweather alilakiwa na raia wa nchi hiyo baada ya kutua. Pacquiao alionekana muda wote akiwa na furaha licha ya maumivu ya upasuaji wa bega pamoja na kutofanya kile alichokidhamiria katika pambano hilo lililofanyika May 2 huko Las Vegas, Marekani na kuweka historia kubwa duniani. Pacquiao alipigwa kwa pointi na mpinzani wake na mara baada ya pambano kuliibuka lawama kuhusu bondia huyo kucheza huku akiwa mgonjwa. Pacqiao amesema hivi sasa atazingatia zaidi kujiuguza bega na kuhakikisha anapona, na baada ya hapo atatangaza kama ataendelea na kibarua chake cha kutwangana mangumi au kustaafu. Mashabiki wake wengi nchini humo walijipanga katika barabara za mji wa Manila na kumlaki shabiki wao. Kufuatia pambano hilo, Mayweather amemuita mpinzani wake mwoga na mshindwaji mkubwa na kutupilia mbali suala la kurudiana naye tena. Lakini kwa upande wake Pacqiao ambaye alishindwa kutangaza, maumivu yake ya bega kabla ya kupigana, amesema atafikiria suala la kupigana nae tena Mmarekani huyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako