• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pep Guardiola huenda akatua Manchester City baada ya Bayern kutokuwa na imani naye

    (GMT+08:00) 2015-05-14 16:17:55
    Staa wa zamani wa Bayern Munich, Lothar Matthaus ameongeza uvumi kwamba kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola atatua Manchester City baada ya kudai kuwa wachezaji wa Bayern hawana imani na kocha huyo. Mhispania huyo amekalia kuti kavu Bayern Munich huku kukiwa na uvumi mwingi kuwa klabu ya Manchester City imeshafikia makubaliano naye ili achukue nafasi ya kocha wao aliyechemsha, Manuel Pellegrini. Tangu achukue ubingwa wa Ujerumani, Bayern imepoteza katika pambano la awali la raundi ya kwanza dhidi ya Barcelona baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 katika dimba la Nou Camp. Lakini pia Bayern ilidundwa katika hatua ya penalti na wapinzani wao wakubwa, Borussia Dortmund katika michuano maarufu ya ndani ya Ujerumani, DFB-Pokal. Bayern pia imepoteza mechi mbili mfululizo za Bundesliga dhidi ya Bayer Leverkusen na Augsburg. Kwa mujibu wa Mtandao wa BeIN Sports imeripotiwa kuwa tayari Guardiola ana makubaliano ya awali ya kujiunga na Manchester City msimu ujao ingawa City imeshindwa kuweka wazi moja kwa moja kuhusu suala hilo. Hivi karibuni Guardiola alikorofishana na daktari wa muda mrefu wa Bayern, Hans-Wilhelm Muller-Wohlfahrt, ambaye aliamua kuachia ngazi klabuni hapo na tangu hapo Guardiola amepoteza marafiki wengi Bayern.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako