• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • La Liga kuendelea kama kawaida bila ya mgomo

    (GMT+08:00) 2015-05-15 11:11:00
    Mahakama kuu ya Hispania imeagiza mechi za ligi kuu nchini humo La Liga ziendelee pasi na mgomo. Mahakama hiyo imeamua kuwa mgomo ulioitishwa na shirikisho la mchezo huo (RFEF) uliodumu kwa juma moja unakiuka vipengee vya makubaliano ya upeperushaji wa mechi hizo. (RFEF) ilipanga mgomo kupinga sera mpya inayopendekezwa na serikali ya kudhibiti mikataba ya upeperushaji wa mechi za ligi hiyo maarufu. Kauli hiyo ya mahakama inaruhusu mechi za ligi kuu zilizokuwa zimesalia kabla ya msimu kukamilika kuchezwa wikiendi hii. RFEF na shirikisho la wachezaji nchini Hispania wamelalamikia kiwango cha chini cha marupurupu watakayopata katika mapendekezo ya mkataba mpya baina ya televisheni ya taifa na serikali. Mashirikika hayo mawili yametofautiana vikali na sera mpya ya kugawanya marupurupu ya fedha za haki miliki ya kupeperusha matangazo miongoni mwa vilabu vyote. Kwa sasa kampuni inayoendesha ligi hii National Professional Football League (LFP) imekubaliana na sera hiyo ya serikali japo wachezaji wanalalamika mapato yao yatapunguzwa. Rais wa LFP Javier Tebas aliahidi kwenda mahakamani kupinga mgomo huo akisema utaigharimu takriban Euro milioni 50 kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako