• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Michuano ya riadha duniani ya Ligi ya Diamond kuanza kutimua vumbi leo Doha

    (GMT+08:00) 2015-05-15 11:13:08
    Michuano maarufu ya riadha duniani ya Diamond League inaanza kutimua vumbi leo Doha, Qatar, huku wakimbiaji nguli kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya kushiriki. Kwa mara ya kwanza katika historia, mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za mita 5,000, Mo Farah kutoka Uingereza naye atashiriki huku akisema anategemea upinzani mkubwa kutoka kwa washiriki. Miongoni mwa wanariadha kutoka Kenya wanaotegemewa kushiriki ni pamoja na Edwin Soi, Thomas Longosiwa na Isaiah Kiplangat Koech. Soi ni mshindi wa medali ya shaba wa mita 5,000 katika michuano ya Olimpiki ya mwaka 2008 iliyofanyika hapa Beijing, wakati Longosiwa naye ni mshindi wa medali ya shaba wa Olimpiki ya London. Kiplangat ni mshidni wa dunia wa mita 5,000 wa medali ya shaba.Yenew Alamirew na Hagos Gebrhiwet kutoka Ethiopia wanategemewa pia kushiriki akiwemo mwana dada Allyson Felix kutoka Marekani. Waandaaji wa michuano hiyo wametenga dola milioni nane kwa ajili ya zawadi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako