• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dau la Goran Kopunovic laitoa jasho Simba

    (GMT+08:00) 2015-05-15 11:13:38
    Baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Simba, kocha Goran Kopunovic ameutaka uongozi kumpa mkataba mpya utakaomwezesha kulipwa Dola 7,500 (Sh milioni 14.6) kwa mwezi. Hali hiyo imekuja baada ya kocha huyo kutoka Serbia kukataa ofa ya kulipwa mshahara wa Dola 5,000 (Sh 9.7 milioni) kwa mwezi kama alivyokuwa akilipwa awali. Kocha huyo ametoa tahadhari kuwa iwapo Simba haitampa mkataba mpya, uongozi wa timu hiyo uwe tayari kuachana naye, waachane na ripoti yake kwa kuwa inaweza isiwe na faida kwa kocha mwingine watakayemleta kutokana na mapendekezo anayoyataka yafanyiwe kazi, lakini pia kutokana na mahitaji yake ya usajili. Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hanspoppe alinukuliwa na mitandao akisema Kopunovic ametaka Dola 50,000 (Sh100 milioni) kama dau la kusaini mkataba na mshahara Dola 8,000 (Sh16 milioni). Kwa upande wake, makamu rais wa klabu hiyo, Geoffrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa klabu yao ina msimamo wa kuendelea na kocha wake (Kopunovic) kwa kuwa wameridhishwa na uwezo wake aliouonyesha ndani ya kipindi kifupi alichofanya kazi kwenye klabu hiyo. Hivi sasa kocha Kopunovic amerudi kwao Serbia na bado haijajulikana kama atarudi kuifundisha klabu hiyo. Habari zisizo rasmi kutoka Simba zinasema kuwa endapo kocha huyo hatakuwa tayari kukubaliana na uongozi, basi watalazimika kutafuta kocha mwingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako