• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Siku ya kimataifa ya jumba la makumbusho

    (GMT+08:00) 2015-05-22 10:09:38

    Mei 18 ni maadhimisho ya 39 ya kimataifa ya jumba la makumbusho. Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Jumba la Makumbusho linafanya juhudi ya kuhimiza maendeleo endelevu ya jamii". Majumba ya makumbusho nchini China yaliandaa shughuli mbalimbali zilizowavutia watazamaji wengi wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

    Shughuli za siku ya jumba la makumbusho ya kimataifa hapa Bejing zinatoa wito wa "Pokezana utamaduni na kujenga siku nzuri za baadaye za taifa." Katika sherehe iliyofanyika kwenye jumba la makumbusho la Beijing, watangazaji wawili maarufu wa televisheni ya taifa ya China CCTV waliteuliwa kuwa Mabalozi wa Jumba la Makumbusho la Beijing, watangazaji hao walisoma shairi lililotungwa kwa ajili ya siku hiyo.

    Licha ya watu wanaoshughulikia mambo ya majumba ya makumbusho, wageni wengi pia walihudhuria sherehe hiyo. Kansela wa ubalozi wa Sudan nchini China, Elrasheed Mohammed Ahmed aliongoza ujumbe wa waandishi wa habari wa Sudan kutembelea jumba la makumbusho la Beijing, akisema jumba la makumbusho ni njia nzuri ya kufahamu historia na utamaduni wa nchi husika. China na Sudan zilikuwa zimeanza kuwasiliana toka zamani sana, sherehe hiyo ilitoa fursa nzuri kwao kufahamu na kujifunza uzoefu wa China.

    "Sudan ina piramidi, pia ina ustaarabu wa kale. Sio tu wakati huu, bali tangu enzi ya kale Sudan pia ilifanya mawasiliano na China. Kama ukifahamu historia ya Mashariki ya Kati, katika enzi ya kale sisi waislamu tulikuwa tunapata ujuzi na elimu kutoka China, ingawa wakati ule China ilikuwa mbali sana nasi. Mtume Muhammad aliwashauri watu wa Mashariki ya Kati kwenda China kutafuta Sayansi na teknolojia mpya. Sasa China imepata tena maendeleo makubwa katika sayansi na teknolojia na ustaarabu. Hivyo tumekuja hapa kutembelea jumba hilo. "

    Sherehe hiyo pia iliwavutia wapenzi wengi wa majumba ya makumbusho. Bibi Rong Xiuxia mwenye umri wa miaka 59 ni mkazi wa Beijing, na ametembelea majumba zaidi ya 100 ya makumbusho jijini Beijing, na pia anafahamu sana historia ya majumba mengi ya makumbusho ya Beijing.

    "Mei 18 mwaka 2006, ambayo ni miaka 9 iliyopita, jumba hilo la makumbusho la Beijing lilifunguliwa kwa mara ya kwanza, nilikuja kulitembelea."

    Kwenye blog yake Bibi Rong alijitambulisha kuwa ana uhusiano wa karibu na jumba la makumbusho, na uhusiano ulianzia mwaka 1987.

    "Mwaka 1987 Beijing ilifanya mashindano ya ujuzi kuhusu jumba la makumbusho, katika muda wa miezi zaidi ya 8 nilitembelea mara kwa mara majumba ya makumbusho. Hivi sasa kama nikisoma habari kuhusu jumba la makumbusho kwenye gazeti, naikata na kuihifadhi. Hizi ni tiketi za majumba mbalimbali ya makumbusho. Nimehifadhi vipeperushi vya majumba mbalimbali ya makumbusho na tiketi zao. Jumba la Makumbusho kweli ni bahari ya ujuzi, kama ukienda mara kwa mara, utalipenda."

    Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 70 ya vita vya pili vya dunia, majumba ya makumbusho hapa Beijing yakishikirisha yameandaa maonesho kuhusu maisha ya watu mashuhuri wanane wa utamaduni katika vita hivyo, ili kuonesha moyo uzalendo wao katika vita dhidi ya uvamizi wa Japani. Naibu mkuu wa Idara ya uhifadhi wa vitu vya kale ya Beijing Bibi Yu Ping anasema, baada ya maonesho hayopia yatafanywa jeshini, shuleni, mitaani na vijijini, hata nje ya China kama vile barani Afrika.

    "Maonesho hayo yanafanywa kutokana na ushirikiano kati ya majumba madogo ya makumbusho na yale makubwa. Jumba la makumbusho la watu hao mashuhuri wanane, kila moja ni dogo sana, lakini linaweza kufanya maonesha kwa kushirikiana na jumba kubwa. Kwa mfano, jumba la makumbusho la mabaki ya mji mkuu wa enzi ya Zhou, ni jumba dogo sana, lakini linaweza kushirikiana na jumba la makumbusho la Beijing na kamati maalumu ya chuo kikuu kutumia vitu vinavyohifadhiwa huko kufanya maonesho. Wanafunzi wengi sasa wanakwenda kutembelea jumba hilo baada ya kutazama maonesho hayo. "

    Mbali na hayo, majumba zaidi ya 30 ya makumbusho yanaandaa shughuli karibu mia moja ili kuwavutia watazamaji wengi zaidi. Bibi Yu anasema,

    "Baadhi ya majumba ya makumbusho yanatunga vitabu vya kiada kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, na kuhamisha darasa la historia katika majumba ya makumbusho, mfano jinsi ya kutengeneza vitu vya kauri, na mchakato wa kutengeneza vifaa vya shaba, wanafunzi wote wataweza kushiriki kwenye utengenezaji. Majumba yote ya makumbusho yanaweza kuandaa shughuli za kuwashirikisha wanafunzi kutokana na vitu vinavyohifadhiwa. "

    Licha ya Beijing, shughuli mbalimbali pia zimefanywa katika sehemu mbalimbali za China. Kwa mfano, kasri la mfalme la Shenyang limepunguza bei ya kiingilio kwa wakazi wa mji huo na kufikia nusu ya bei ya kawaida. Jumba la makumbusho mkoani Hunan limeonyesha filamu ya katuni inayotengenezwa na jumba hilo, na chama cha wafanyabiashara wa China wanaoishi nchini Kenya pia kinaleta sanamu za vinyago kuoneshwa kwenye jumba moja la makumbusho huko Ningbo, kusini mwa China. Mwakilishi wa chama hicho Bibi Yang Feifei anasema,

    "Maonesho ya sanamu za vinyago yanayoandaliwa na chama chetu yanafunguliwa leo huko Ningbo. Vinyago hivyo vina historia ya zaidi ya miaka 200, baadhi yao tuliyakusanya kutoka makabila mbalimbali, na vingine vimetolewa na serikali ya Kenya. Vinyago hivyo vinaweza kuonesha utamduni wa wakenya. Sisi wachina tunasema, binadamu hutoka ardhi na kurudi kwenye ardhi. Na makabila ya Kenya yanasema, uhai wa binadamu unatoka kwenye maji, na kurudi kwenye maji, hivyo vinyago vya Afrika vinaonesha uhusiano kati ya uhai na maji."

    Jumba la Makumbusho sio tu linajenga daraja kati ya utamaduni tofauti, bali pia linaandika historia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako