• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza aanza ziara barani Ulaya ili kuhimiza mageuzi ya Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2015-05-29 10:45:03

    Rais Francois Hollande wa Ufaransa amempokea waziri mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron, ambaye yuko ziarani barani Ulaya ili kutetea mageuzi ya Umoja wa Ulaya kabla ya kura za maoni zinazotarajiwa kufanyika kabla ya mwishoni mwa mwaka 2017 nchini Uingereza kuamua kama nchi hiyo itaendelea na uwanachama wake wa umoja huo.

    Rais Hollande amesema Ufaransa inaitaka Uingereza ibaki katika Umoja wa Ulaya. Amesema Bw. Cameron atatoa mapendekezo yake na watayajadili.

    Awali, Bw. Cameron alitoa mwito kwa wenzake wa Ulaya kuunga mkono mageuzi ambayo si kama tu yatainufaisha Uingereza, bali pia nchi nyingine za Ulaya. Baada ya ziara yake nchini Ufaransa, Bw. Cameron pia atakwenda Poland na Ujerumani kukutana na waziri mkuu wa Poland Ewa Kopacz na chansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako