• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA kufanyika leo

    (GMT+08:00) 2015-05-29 10:53:48

    Mkutano wa Baraza Kuu la 65 wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA ulifunguliwa jana huko Zurich, Uswisi kwa lengo la kuchagua viongozi wapya, ikiwa ni pamoja na mwenyekiti wa Shirikisho hilo. Hata hivyo mkutano huo umegubikwa na msukosuko baada ya maofisa saba waandamizi wa Shirikisho hilo kukamatwa baada ya Marekani kuwafungulia mashtaka ya makosa ya udanganyifu, rushwa na kusafisha pesa.

    Wagombea wawili Bw Sepp Blatter ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa FIFA na Prince Ali Hussein wa Jordan wanapewa nafasi ya kushinda kwenye uchaguzi huo. Lakini jana mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA BW Michel Platini alimtaka Bw Blatter ajiuzulu kutokana na kashfa za ufisadi, baada ya Bw Blatter kukataa kujiuzulu Bw Platini alisema UEFA itamuunga mkono Prince Bin Ali, na kuwashauri wengine kufanya hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako