• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya BRAZIL yaipa kenya mkopo wa sh bilioni 7.9 kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo nchini kenya.

    (GMT+08:00) 2015-05-29 20:34:53

    Serikali ya BRAZIL imekubali kutoa mkopo wa sh bilioni 7.9 kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo nchini kenya.

    Mkuu wa biashara kutoka Brazil nchini Kenya Victoria Balthar, anasema serikali yake imeidhinisha mkataba wa makubaliano kati ya nchi hizo mbili, ambayo itaiwezesha Kenya kupokea mkopo wa Sh bilioni 7.9 kwa ajili ya mashini za kilimo nchini.

    Mkataba huo ulisainiwa mwaka jana kati ya wizara ya kilimo, wizara ya maendeleo, viwanda na biashara ya nje ya Brazil, chini ya Mpango wa Kimataifa wa Chakula Zaidi. (maarufu kama 'Mais Alimentos Programa').

    Chini ya mpango huo, Brazil itatoa mikopo kwa nchi za Afrika kufadhili vitega uchumi kwa ajili ya kilimo cha wakulima wadogo wadogo, kwa lengo la kuboresha uzalishaji wa chakula na kipato cha jamii za vijijini.

    Fedha hizo pia zitapeanwa kwa njia ya mikopo kwa wakulima wadogo ili kuwezesha kukununua mashini mpya za kilimo na vifaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako