Waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki Nikos Kotzias amesema, karibu fedha zote za msaada zilizopokewa na nchi hiyo zimetumika kulipa madeni. Waziri huyo anasema
"Asilimia 96 ya fedha tulizopokea katika miaka sita iliyopita tumezitumia kuwalipa wadeni wetu. Hii ina maana kuwa, ninakupa hela ili unipe tena mimi, na nataka wewe ujisikie vibaya kwa kuharibu mshikamano niliodai. Wamefanikiwa kupata fedha zao na kuziambia nchi za Ulaya kuwa wataishi kwa mshikamano"
Ugiriki na wadeni wake wanaendelea na mazungumzo kuhusu makubaliano ya 'fedha kwa mageuzi', lakini kuna taarifa kuwa pande hizo huenda hazitafikia makubaliano kabla ya jumapili, siku ya mwisho iliyowekwa ya kufikia makubaliano na kutolewa msaada wa fedha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |