• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matunzo ya uzeeni

    (GMT+08:00) 2015-06-21 18:31:52

    Kutokana na maendeleo ya huduma za afya, lishe na hata maisha kwa ujumla, kwa sasa wachina wanaishi kwa muda mrefu zaidi kuliko zamani. Lakini kutokana na mchanganyiko wa mabadiliko ya muundo wa familia za China na ongezeko la idadi ya wazee, jamii ya China imefikia hatua ya kuanza kuangalia namna ya kuwatunza wazee, hasa wale ambao umri wao ni mkubwa sana na hawawezi kujitunza, hali ambayo ni tofauti na mfumo wa jamii wa jadi yaani kutunzwa na wanafamilia. Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka juzi idadi ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 ilifikia milioni 212, ambayo ni zaidi ya asilimia 15 ya watu wote wa China, na idadi hiyo inatarajiwa kuendelea kuongezeka kwa watu milioni 10 kila mwaka. Ongezeko hili la idadi ya watu ni kubwa, na haliwezi kupuuzwa. Sababu ni kuwa muundo wa familia za China umebadilika, kwa sasa hakuna mfumo imara wa jadi wa kuwatunza wazee, kwa hiyo China inatakiwa kutumia njia mpya kuwatunza wazee hao. Njia ambazo jamii ya China haijazoea na ambazo kimsingi haziendani na utamaduni wa jadi wa China. Kwa undani zaidi hebu sikilizeni kipindi chetu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako