• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kipindi maalum cha tatu kuhusu Siku ya Albino ya Kimataifa--Hatma yetu sio ndoto

    (GMT+08:00) 2015-07-24 11:05:03

    Katika vipindi viwili vilivyopita tumezungumzia kadhia, au adha wanazokutana nazo Albino. Tulianzia nchini Tanzania na Kenya, tukazungumzia hali ya Albino hapa China, na katika kipindi cha leo, tunazungumzia "Hatma yetu sio ndoto".

    Katika miaka kadhaa iliyopita, Albino wengi waliuawa kila mwaka, wengi wao ni watoto ambao hata hawakutimia mwaka mmoja. Baada ya kuuawa, viungo vyao vilikatwa na kuuzwa kwenye masoko haramu, kama nyongeza ya dawa za kienyeji na kwa kujilinda. Viungo hivi vinauzwa bei ghali sana, habari zinasema kuwa, bei ya kiungo cha albino imefika dola za kimarekani zaidi ya elfu 3. Masoko hayo yako sehemu nyingi za Afrika mashariki, watu wengi wanafanya biashara hii ingawa ni ya hatari sana.

    Lakini ukiangalia kwa undani maisha ya Albino, utagundua kuwa hawana shinikizo, bali wanaishi kwa matarajio makubwa, wengi wao hata wanapambana kwa ushujaa na vitendo vya mauaji ya kinyama na ubaguzi. Mwenyekiti wa shirikisho la albino la Mwanza, Tanzania Bw. Alfred Kipole ni mmojawapo.

    "Mimi nilijaribu kusaidia serikali nilijitolea baada ya mtu kuniomba nywele, nikasema niweke mtego huo ili tuweze kubaini ni wangapi wanaofanya vitu hivi, baada ya kuandaa mtego huo serikali iliweza kukamata ikaweka kielelezo baada ya kunyoa nywele zangu na kumkabidhi huyo mtu na baadaye wakambaini huyo mtu."

    Lakini familia nyingi zenye watoto albino haziwaachii watoto wao.

    "Ukiwa na mtoto albino, unasikia nini?"

    "Nasikia vizuri."

    "Ngozi ya baba yake ni rangi gani?"

    "Yeye ni mweusi, watoto albino wanafanana na watoto wengine."

    Watoto Albino ni sawa na watoto wengine, tofauti ni rangi, nywele, na uwezo wa kuona. Wakati huo huo, watu wengi wenye nia njema wanafanya juhudi kwa ajili ya kuondoa ubaguzi dhidi ya albino. Oscar Haule ni mfanyabiashara wa Tanzania, yeye si albino, lakini aliamua kuwasaidia watu hao kwa kuwa anawaona ni sawa na watu wengine, wala sio waovu. Wakati kombe la dunia lilipokaribia kufanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza, alipata wazo la kuunda kikosi cha mpira wa miguu, ambacho wachezaji wote watakuwa ni albino, alitaka kufanya hivyo ili kuthibisha kuwa wanafanana na watu wa kawaida, na hata wanaweza kufanya vizuri zaidi.

    Oscar aliamua kukiita kikundi hicho kuwa "Muungano wa Albino", na anatumai kuwa, wakati mpira wa miguu barani Afrika utakapokuwa habari muhimu ya kwanza duniani, "Muungano wa Albino" pia utashangaza watu.

    "Hebu tuunge mkono 'Muungano wa Albino'. Tunawalika vijana kujiunga nasi, tunahitaji uungaji mkono wa jamaa na watu wote, tunapinga mauaji yaliyotokea awali"

    Timu hiyo ilianzishwa haraka, na mashindano yalianza, wachezaji wote walijitahidi na kujipatia haki zao kupitia miguu yao, na kutaka kubadilisha maoni ya watu ya awali. Oscar pia alimwalika mtengeneza filamu maarufu Nick Broomfield kurekodi mashindano ya mwanzo yaliyochezwa na "Muungano wa Albino".

    "Wamefanya vizuri leo. Mwanzano ulionyesha mvua, tulikumbwa na tatizo. Ni nguvu kucheza mpira katika matope. Lakini ndiyo hiyo iliongeza burudani ya mashindano hayo. Upande wowote unawezekana kupata ushindi, lakini mwisho tumekuwa washindi"

    "Muungano wa Albino" ulipata ushindi katika shindano moja baada ya jingine, watu kote nchini Tanzania walianza kuwafuatilia, na kuwafuatilia albino.

    "Watu wengi wameanza kupokea who I am sasa. Nikiwa mgonjwa wa albino, nina nafasi chache sana kuliko wengine. Lakini timu yetu inayoshirikishwa na wagonjwa wa albino, imetimiza lengo letu la pamoja."

    Msimu wa kwanza wa mashindano umemalizika, na "Muungano wa Albino" umechukua nafasi ya 4.

    "Leo tutaandikwa kwenye historia, naona furaha kuwa Maulidi amepata mabao mawili, Hali pia amepata bao. Nitalala unono."

    "Muungano wa Albino" unatumai kubadilisha maoni ya watu kutokana na ushindi wao, na watafanya kila liwezekanalo kutimiza hilo. Jambo la kufurahisha ni kuwa, rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ameahidi kuwa, atazuia kuongezeka na hata kutokomeza mauaji ya albino nchini mwake. Hivi sasa askari polisi wa Tanzania wameanza kutoa ulinzi kwa watoto albino wakiwa njiani kutoka shule hadi majumbani kwao, na biashara ya viungo vya albino pia imepigwa marufuku. Serikali ya Tanzania pia imetangaza kuwa, itaweka kumbukumbu husika za kila Albino nchini humo, juhudi ambazo zimewafurahisha Albino na kuona kuwa maisha mazuri ya baadaye waliyoyatamani kwa muda mrefu yanawezekana.

    Kwa upande wa Kenya, kutokana na wito uliotolewa na jumuiya ya kimataifa na juhudi zinazofanywa na albino, serikali ya nchi hiyo inazingatia zaidi siku hadi siku uhifadhi wa haki zao, na imeanza kutunga sheria husika. Mbunge Isack Mwaura ambaye ni albino anaona kuwa, mafanikio yaliyopatikana leo yanatokana na kutokubali kushindwa, bila kujali anafanya kazi gani, anafanya kila awezalo kupata haki kwa albino, na Kenya inatarajiwa kujifunza kutokana na juhudi za Tanzania katika kuwalinda albino.

    "Tanzania imetoa uzoefu kwa Kenya katika kupitisha sheria husika za kuadhibu kuwaua wagonjwa wa albino kwa visingizio vya utamaduni na dini. Zaidi ya hayo, nikiwa mbunge, moja ya kazi zangu ni kufanya wagonjwa wote wa albino nchini Kenya wapewe cream ya kinga ya juakali kwa bure. Vilevile wapewe sunglass, kofia, na kufutwa gharama za masomo. Hivi sasa shirikisho langu linagharamia masomo ya watoto 14."

    Jumuiya ya kimataifa vilevile inafanya juhudi kuwapatia Albino haki na ulinzi. Mfuko wa kuhudumia watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF, na Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa zimejiunga na juhudi hizo, ambazo kwa sasa zinashirikiana na serikali na idara husika za Kenya na Tanzania, ili kuzuia vitendo vya kikatili dhidi ya albino. Kamati ya haki za binadamu ilipitisha azimio husika mwezi Machi na kumteua ofisa maalum atakayeshughulikia kutoa ripoti kwa kamati hiyo kuhusu haki za albino, na changamoto zinazowakabili kwa miaka mitatu. Ofisa huyo pia anatarajiwa kuwasiliana na serikali za nchi husika kuhusu kuhimiza haki za albino, pamoja na usawa wao katika jamii.

    Hapa China, hakuna mauaji dhidi ya albino, lakini Albino hao wanafuatilia sana hali ya wenzao barani Afrika. Mwanzilishi wa shirikisho la "familia ya watoto wa mwezi" la China Guan Lu anasema "Sisi sote ni watoto wa 'mwezi'!"

    "Natumai tunaweza kuwa na mawasiliano zaidi kuhusu habari, albino ni kundi maalum. Nadhani albino nchini Tanzania na Kenya, wanatumai kuwasiliana na wenzao walioko sehemu nyingine. Kama utaratibu ukifikiwa, tutaweza kuwahamasisha "watoto wa mwezi" hapa kwetu kuwasaidia wenzao wa huko, juhudi hizi zinatarajiwa kufanywa katika siku za mbele."

    Guan Lu anafahamu vizuri historia ya "Muungano wa Albino".

    "Vedeo hii inaeleza hadithi za albino nchini Tanzania. Tulitafuta watu waliojitolea, wakaitafsiri kwa Kichina, na tuliiweka kwenye tovuti ya internet na kufanya matangazo fulani juu ya video hiyo."

    Guan Lu alituambia, baada ya kuwasiliana na familia nyingi za albino, aliwashukuru wazazi wake, kwani walimwambia kuwa anafanana na watoto wengine, isipokuwa yeye ni mweupe zaidi. Anafurahi kuona kuwa, familia nyingi zaidi siku hadi siku zinatenga mazingra bora yenye furaha kwa watoto wao wa albino, na kuwaunga mkono wajitahidi kutimiza ndoto zao.

    Wang Jiahe ni mwanachama shabiki kwenye "familia ya watoto wa mwezi", hajawahi kukosa hafla yoyote ya familia hiyo. Uwezo wake wa kuona ni 0.02 tu, lakini anajisikia mwenye bahati, kwani anapenda kucheza piano tangu utotoni, anaungwa mkono na watu wote walio karibu naye, na angependa kuwashukuru.

    "Nataka kuwashuruku sana bibi na mwalimu wangu. Ninajifunza piano, mwalimu wangu alikuwa ananitunza tangu utotoni, hunifundisha kwa uvumilivu mkubwa, na bibi pia ananiunga mkono."

    Kutokana na maneno ya bibi Qiao, tunaweza kuhisi furaha yake na jinsi anavyoguswa.

    "Mwalimu huyu anamchukua vizuri, hawezi kuona vizuri, hiyo kila alipocheza piano, anaruhusiwa kusimama mbele ya blackboard. Tangu wakati ule hadi sasa, ada ya mwalimu huyo ni yuan 40 tu kwa kila somo, ambayo ni kidogo sana. Mwalimu huyo anafanya mchango wake, na sisi tunabidi kufanya juhudi kubwa tuwezavyo. Familia yetu ni ina amani, mazingira nyumbani ni mazuri sana."

    Barani Afrika au nchini China, mazingira mazuri au mabaya, watu hawa wa kawaida wanapiga hatua mbele siku hadi siku katika kutimiza ndoto zao.

    "Uone nilikuambia nini. Tumethibitisha nyinyi mmekosea. Harambee, 'Muungano wa Albino'."

    "Anataka kushiriki kwenye mashindano ya piano ya taifa baada ya miaka mitatu, tutaangalia kama tutaweza au la."

    "Nataraji mtoto wangu, awe na furaha, hii ni jambo zuri zaidi."

    "Mimi nina umri wa miaka 30 kwa sasa, natarajia nitapata mchumba wangu na tutaishi maisha yetu yote, tutaoana. Hali halisi ni kuwa, naishi vizuri sasa, natumai sisi sote tutaishi vizuri."

    Mwisho tungependa kuwashukuru wasikilizaji wetu wote kwa kutusikiliza. Vilevile tungependa kupokea maoni yenu kuhusu kipindi hiki cha leo, na mnaweza kutuma maoni hayo kwa njia ya facebook anuani yetu ni www.facebook.com/kiswahilicri, au kwa njia ya simu namba yetu ni +8615611015572, pia unaweza kukutumia kwenye tovuti yetu, tunathamini michango na maoni yako.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako