• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tunisia yatangaza hali ya dharura kufuatia shambulizi dhidi ya hoteli mjini Sousse

    (GMT+08:00) 2015-07-05 20:06:23

    Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi jana alitangaza hali ya dharura ya nchi, kufuatia shambulizi lililotokea wiki iliyopita dhidi ya hoteli moja mjini Sousse ambalo lilisababisha vifo vya watalii 38 wa kigeni, wengi wao raia wa Uingereza.

    Tarehe 26 Juni, Seifeddine Rezgui, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23 alishambulia hoteli ya Marhaba huko Sousse kwa kutumia bunduki, na baadae akauawa kwa risasi na walinzi wa usalama kilomita kadhaa kutoka kwa hoteli hiyo.

    Tawi la kundi la IS nchini Libya limetangaza kuhusika na shambulizi hilo na kwamba litafanya mashambulizi zaidi nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako