• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujumbe wa IAEA wawasili nchini Iran kwa majadiliano ya ushirikiano wa pamoja

    (GMT+08:00) 2015-07-06 18:13:13

    Ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA umewasili kwenye mji mkuu wa Iran, Tehran, kwa ajili ya majadiliano ya kina kuhusu makubaliano ya ushirikiano kati ya Iran na Shirika hilo ili kusuluhisha masuala ambayo bado hayajafikiwa makubaliano katika suala la mpango wa nyuklia wa Iran.

    Msemaji wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Behrouz Kamalvandi amesema, ujumbe wa IAEA utajadili utekelezaji wa ratiba ya ushirikiano na maofisa wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran.

    Kwa muda mrefu IAEA imeitaka Iran kutoa kibali kwa wachunguzi wake kutembelea maeneo ya kijeshi ili kuthibitisha kama vitendo vyovyote vinavyohusiana na nyuklia vimefanyika, ombi ambalo Iran inaliona sharti limezidi Makubaliano ya Kuondoa Silaha za Nyuklia na wajibu wa Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako