• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zalisheni asali kwa wingi: Aomba Pinda.

    (GMT+08:00) 2015-07-06 20:25:50

    Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amewataka warinaji asali nchini Tanzania kuwekeza zaidi katika sekta hiyo kwa kuwa nchi hiyo ina uwezo zaidi wa kuzalisha asali kwa wingi na kuuza katika mataifa ya nje.

    Pinda akizungumza katika maonyesho ya kibiashara ya Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki amesema kuwa taifa hilo limekuwa likizembea katika uzalishaji wa bidhaa hiyo wakati ambapo limo katika fursa nzuri ya kufanya vyema zaidi hata kuliko Uhabeshi ambayo uzalisha asali kwa wingi katika kanda hii.

    Hata hivyo Pinda amewataka warinaji asali kuchukua fursa ya kupata masomo kuhusiana na sekta hiyo ili kutoa bidhaa zilizo na ubora wa kimataifa.

    Miaka kadhaa iliyopita nchi hiyo ilikuwa imesimamisha uuzaji wa bidhaa hiyo nje ya taifa hilo kutokana na lalama za kudorora kwa ubora wake.

    Wakati huo huo amewataka wakulima kwa ujumla nchini humo kuchamngamkia kilimo kwa kuwa sekta hiyo ina fursa nyingi za kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako