• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya saruji ya CIMERWA nchini Rwanda yazindua kiwanda kipya.

    (GMT+08:00) 2015-07-13 19:28:52

    Kampuni kubwa zaidi ya saruji nchini Rwanda ya CIMERWA imezindua kiwanda kipya katika eneo la Rusizi, kiwanda ambacho kinatarajiwa kuzalisha saruji ya kuuza katika mataifa ya kanda.

    Sasa kiwanda hicho ambacho ni cha kipekee katika nchi hiyo kinatarajiwa kuongeza uzalishaji wa saruji nchini Rwanda kutoka tani 100,000 kwa mwezi hadi tani 600,000.

    Kaimu afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Juvenal Rutaganda anasema kwa sasa kiwanda hicho kitazalisha saruji ya kutosha nchini Rwanda na ziada yake ya tani 350,000 kila mwaka kuuzwa katika mataifa jirani kama vile Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi.

    Kulingana na wachanganuzi wa kibiashara ni kwamba pia kuongezeka kwa uzalishaji wa saruji katika taifa hilo huenda kukapunguza bei yake jambo ambalo limekaribishwa na wateja.

    Nao vijana nchini humo wamechangamkia fursa za kazi katika kiwanda hicho na kulingana na Juvenal ni kwamba wanatarajia kuwaajiri vijana zaidi katika siku za usoni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako