• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utamaduni wa harusi za wachina wabadilika kwa kuendana na wakati

    (GMT+08:00) 2015-07-16 15:43:28

    Harusi ni moja ya sherehe muhimu katika maisha ya karibu watu wote duniani, ambayo inaonesha mapenzi kati ya wanandoa na pia kuthibitisha wajibu na majukumu yao katika ndoa. Kila nchi na taifa lina utamaduni wake wa jadi kuhusu harusi, lakini mila na desturi hizo pia zinabadilika kwa kuendana na wakati.

    Nchini China, rangi nyekundu inatumika kwenye harusi ya kijadi, kwa kuwa wachina wanaamini kuwa rangi hiyo inaonesha furaha, na inaleta bahati nzuri na neema. Nyumba ya harusi inatakiwa kupambwa kwa mapambo yenye rangi nyekundu, kama vile kubandika karatasi nyekundi zenye maandishi ya kichina Xi, maana yake ni Neema. Bibi na bwana harusi wanatakiwa kuvaa nguo za jadi za rangi nyekundu, na maua ya rangi nyekundu kifuani. Bibi harusi pia anatakiwa kufunika sura yake kwa kitambaa chekundu, kabla ya kuingia kwenye kiti kilichofunikwa kwa mapambo kinachobebwa na watu, ambacho kwa kichina kinaitwa "Jiaozi". Kwenye harusi ya jadi nchini China, bibi harusi hatembei mwenyewe, anatakiwa kubebwa kwenye kiti hicho kutoka nyumbani kwao hadi nyumbani kwa bwana harusi, halafu bwana harusi atafunua kitambaa hicho, ili kuwaonesha ndugu zake sura ya bibi harusi.

    Hiyo ni harusi ya jadi nchini China, kutokana na utandawazi wa kiutamaduni duniani, harusi za vijana wa China nazo zimeanza kuchanganya mitindo ya kigeni. Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, mara baada ya China kutekeleza mageuzi na kufungua mlango kwa nje, harusi ilikuwa rahisi tu, wanandoa wapya huandaa sherehe na tafrija ndogo, wengine waliamua kufanya utalii wenyewe badala ya sherehe ya harusi.

    Wakati huo, gharama za harusi zilikuwa chini, hata yuan mia kadhaa zilikuwa zinatosha kabisa. Mahari ya bibi harusi pia haikuwa kubwa, watu wa wakati huo walipendelea saa, baiskeli, cherehani na radio, hata masofa walitengeneza kwa mafundi seremala. Picha za harusi za miaka ya 80, ni tofauti na za sasa. Picha hizo zilikuwa za rangu nyeusi na nyeupe, na huwa zilipigwa ndani ya studio ya kupigia picha.

    Tukiingia miaka 90 karne iliyopita, vijana walipendelea tena harusi za jadi za kichina, lakini walifanya sherehe za harusi kwenye hoteli za kifahari. Baadhi ya vijana wanaopenda mtindao wa maisha ya magharibi walifanya harusi zao za kimagharibi kwenye ukumbi wa kanisa. Gharama za harusi ziliongezeka kulingana na za miaka ya 80, asilimia 73 ya harusi ziligharimu zaidi ya dola za kimarekani 1,600, na asilimia 27 ya harusi zilitumia zaidi ya dola za kimarekani 4,800. Kwa upande wa mahari, vijana wa wakati huo walipendelea vifaa vya umeme vya nyumbani, kama vile televisheni za rangi, kiyoyozi, mashine ya kufulia, na jokofu, na pia walianza kutilia maanani mapambo ya ndani. Wakati huo, picha za harusi zilikuwa zinachanganya na mtindo wa kimagharibi, yaani bibi harusi huvaa gauni jeupe la harusi na bwana harusi huvaa suti.

    Baada ya kuingia karne ya 21, harusi zimekuwa za aina mbalimbali, jadi kwa kisasa, rahisi kwa fahari, na hata kuna zile zinazokusudia kuvunja rekodi ya dunia. Wakati huo, katika miji 30 mikubwa nchini China ikiwemo Beijing, Shanghai, Nanjing na Dalian, wastani wa wanandoa wapya milioni 3.73 walitumia zaidi ya dola za kimarekani elfu 20 katika harusi zao, ikiwa ni gharama ya sherehe pekee, kama zikiwekwa pamoja gharama za kununua nyumba na magari, kwa jumla harusi katika miji ya Shanghai, Beijing na Hangzhang itazidi dola za kimarekani laki 1.6, na kwa sehemu za pwani, inafikia dola za kimarekani elfu 64. Wakati huo, nyumba imeanza kuwa sehemu muhimu ya mahari, na pia ni mzigo mkubwa kwa wanandoa na hata familia zao. Kutokana na kuathirika na tamaduni kutoka nje, vijana wa karne mpya wanapendelea picha za harusi zenye ubunifu, kama vile picha za harusi kwenye vilele vya milima ya theluji au chini ya maji.

    Ripoti ya uchunguzi kuhusu sekta ya harusi nchini China kati ya mwaka 2006 hadi 2007 inaonesha kuwa, wakati huo wastani wa gharama za harusi ilizidi dola za kimarekani elfu 19. Kwa mfano mjini Shanghai, katika nusu ya kwanza ya mwaka 2006, wastani wa gharama za harusi ilizidi dola za kimarekani elfu 25, ambayo iliongezeka kwa mara tatu kuliko miwaka mitatu iliyopita.

    Hiyo ni hali ya mijini, kwenye sehemu za vijijini, gharama za harusi ni mzigo mkubwa zaidi zikilinganishwa na mapato yao. Mtaalamu wa mambo ya ndoa na harusi nchini China Bi. Li Yinhe amesema, gharama ya harusi ni kama mara 10 ya pato la jumla la familia kwa mwaka mmoja. Kijana Liu Jian anatoka kijiji kimoja wilayani Daokou katika mji wa Anyang mkoani Henan, sasa anafanya kazi za vibarua mjini Beijing. Anasema, hivi sasa harusi kijijini kwake hugharimu dola za kimarekani elfu 32 hadi elfu 48, lakini pato la jumla la familia nzima katika mwaka moja ni dola za kimarekani 300 hadi 500 tu.

    Tofauti na hali ya zamani, harusi za leo ni kama maonesho makubwa. Wanandoa wapya wanashindana ufahari wa harusi zao, jambo lililoifanya sherehe hiyo kuwa mzigo mkubwa wa kifedha kwa familia za pande zote mbili. Je,kweli inastahili?

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako